
Klabu ya Simba Sc ya Tanzania Leo inatupa karata yake ya pili ya michuano ya kimataifa itakapomenyana na Jwaneng Galaxy ya Botswana jioni ya Leo katika michuano ya Klabu bingwa Afrika. Katika mchezo wa Kwanza uliochezwa Botswana Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 hivyo leo ushindi wowote au sare inatosha kuipeleka Simba hatua ya makundi. Hadi kufikia Sasa Simba ndo Klabu pekee nchini Tanzania iliyosalia katika michuano ya kimataifa baada ya Yanga, Azam, na Biashara kutupwa nje ya mashindano.je Simba wataibeba Tanzania ama la. Majibu tutayapata katika dimba la Mkapa jijini Dar es salaam majira ya saa kumi jioni